Mwaka huu daima utakubukwa na wengi hasa kwa matukio mengi yamekuba raia wa nchi ya kenya.
Mwisho wa mwaka uliopita mamilioni ya wakenya walijitokeza kupiga kura kuchagua viongozi watakaowangoza miaka mitano.Wengi wao hawa kutaraji kuwa wangeweza kuwa wakibizi katika nchi yao, nchi jirani na kuwa wangeadhibiwa kwa kushiriki katika demokrasia.
Jumla ya wakenya elfu moja mia tano waliuwawa na wengine laki mia nne kufanywa wakibizi. Maeneo yalioadhiriwa sana ni yale ya mkoa wa bonde la ufa, mkoa wa magharibi,na mkoa wa pwani.
Uchumi ulizorota huku sekta za utalii,kilimo,usafiri na elimu zikiadhiriwa sana.Makabira yaliyoishi kama ndugu sasa yalibadirilika na kuwa maadui na kuuana kama kuku.
Katibu wa zamani wa umoja wa mataifa, Koffi Annan alihitajika kuunganisha pande zilizokuwa zikizozana.Mwisho pande hizi zilikubaliana kuuunga serikali ya umoja wa kitaifa.
Mwezi wa mei wakenya walioishi Afrika Kusini walijipata mashakani waliposhabuliwa na raia wenye hasira, kwa madai kuwa wamewapokonya nafasi zao za kazi.Jumla ya raia elfu kumi wa kenya wamejipata matatani wakishabuliwa kwenye ghasia hizo huku wengi wakitoroka na kurundi nchi yao.
Raia walioadhiriwa sana ni wazimbabwe na msubiji. Inakisiwa kuwa kunajumla ya wakaazi wakigeni milioni tano Afrika Kusini.
Friday, May 23, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment