Saturday, April 19, 2008

UCHAGUZI WARUDIWA MAKERERE



Siasa za Kenya zimevuka mipaka hadi nchi jirani ya Uganda.Uchaguzi wa chama cha wanafunzi wa jamii ya wakenya chuo cha makerere ulivurugwa siku ya jumapili na sasa ni halali utafanyika siku ya jumanne wiki ijayo.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na tume ya uchanguzi inayoongozwa na Fredrick Obondo uchaguzi utafanyika tarehe ishirini na moja mwezi huu katika uwanja mkuu wa uhuru wa chuo.

Wagombea tofauti katika chadhifa mbalimbali wanaendelea na shughuli za mwisho za matayarisho ya uchanguzi huku wengine wakiungana. Nyadhifa ambazo zinaupinzani mukali ni zile za uraisi ambazo zimevutia wagombea sita lakini wabashiri wanatabiria upinzani kati ya Birghen Kiplimo Eliud, Ibrahim Shukri na Pyhilis Wangare.

Uchaguzi huo ulitibuka siku ya jumapili baada ya mvua kubwa kunyesha na kutibua shughuli hiyo.

Polisi wanatarajiwa kushika doria siku hiyo kuimarisha doria na kuzuia rabsha.

Tuesday, April 1, 2008

KAMPENI YA CHACHA

Jamii ya wanafunzi yakutoka Kenya chuo cha Makerere Imeimarisha Kampeni ya kutafuta atakaye kuwa Raisi wa chama kijulikanalo kama Makerere University Kenya Students Association(MUKESA) kwa kimombo, uchanguzi unatarajiwa kuwa katikati mwa mwezi huu.

Jumamosi iliyopita, jumla ya wanafunzi mia nne walijitokeza ili kuchagua tume ya uchanguzi itakayo simamia uchaguzi huo.Fredrick Obondo aliibuka mshindi kwa kuzoa kura mia moja na ishirini,akifuatwa kwa karibu na Fredrick Orere na kura 118,jotham Gaitho akapata kura arobainne na nane.

Kufikia sasa wagombea uchanguzi wanne wamejitokeza. Birghen Kiplimo Eliud,Nganga ,Shukri,Joel.

Wengi wamewaraumu wagombea uchanguzi kwa kufanya kampeni wakijivizia kabila zao.